Tangu enzi za zama,
kabla kuzaliwa baba na mama,
Hakuna mtu aliyezama,
kuelekea kwa mama pima,
Babu alitoka huku
akikwama, aghalabu kuhitaji rukwama,
Nyumbani alifika
salama, kupunguzia nyanya gharama.
Vivyo hivo walifanya,
walofuata baadae,
Kila siku baba
alipenya, asiwaache wanae,
Mama naye kutukanya,
pombe heri ikae,
Hayo yote
yalinifinya, Athumani niokolee.
Mtu angenipa pombe ya
kale, singesita kuikunywa,
Kwa sababu wakati
ule, haikuwa shida kwa kinywa,
Nakumbuka pombe ile,
ilihitaji kufinywa,
Ili ifike kiwango
kile, kisohitaji kukanywa.
Lakini tembo ya siku
hizi, jameni ina mikosi,
Kumbuka hivi juzi,
ilivyochukua roho kasi,
Mama atokwa na chozi,
mtoto kajaa kamasi,
Baba yetu kafa ja
mwizi, kalazwa kama mjusi.
Ole wenu mnayofanya
haya, ona kaenda tulomtegemea,
Hata hamwoni haya,
kunambia nyasi itamea,
Nawe ulozoea kaya,
nami basi nakukemea,
Chunga usikanyage
nyaya, nao ukauke mmea.
©2014. All Rights Reserved @Abedos Media.
No comments:
Post a Comment