say it all

I always say it all as it comes/happens depending on the magnitude!

Thursday 22 May 2014

Mama Pima




Tangu enzi za zama, kabla kuzaliwa baba na mama,

Hakuna mtu aliyezama, kuelekea kwa mama pima,

Babu alitoka huku akikwama, aghalabu kuhitaji rukwama,

Nyumbani alifika salama, kupunguzia nyanya gharama.

Vivyo hivo walifanya, walofuata baadae,

Kila siku baba alipenya, asiwaache wanae,

Mama naye kutukanya, pombe heri ikae,

Hayo yote yalinifinya, Athumani niokolee.

Mtu angenipa pombe ya kale, singesita kuikunywa,

Kwa sababu wakati ule, haikuwa shida kwa kinywa,

Nakumbuka pombe ile, ilihitaji kufinywa,

Ili ifike kiwango kile, kisohitaji kukanywa.


Lakini tembo ya siku hizi, jameni ina mikosi,

Kumbuka hivi juzi, ilivyochukua roho kasi,

Mama atokwa na chozi, mtoto kajaa kamasi,

Baba yetu kafa ja mwizi, kalazwa kama mjusi.

Ole wenu mnayofanya haya, ona kaenda tulomtegemea,

Hata hamwoni haya, kunambia nyasi itamea,

Nawe ulozoea kaya, nami basi nakukemea,

Chunga usikanyage nyaya, nao ukauke mmea. 


©2014. All Rights Reserved @Abedos Media.